Monday, July 4, 2016

NANI HUYOO VALENCIA

WINGA wa Portugal Nani, ambae Jumatano Usiku ataiwakilisha Nchi yake kwenye Nusu Fainali ya EURO 2016 dhidi ya Wales, amejiunga na Valencia ya Spain kutoka Fenerbahce ya Uturuki na kusaini Mkataba wa Miaka Mitatu.
Valencia imethibitisha Uhamisho huu bila kutoa idadi ya Ada ya Uhamisho baada ya kutoa Taarifa kwenye Tovuti yao ikisema Luis Carlos Almeida – 'Nani' – Mchezaji wa Kimataifa wa Portugal atakuwa na wao kwa Miaka Mitatu.

Valencia imefanikiwa kumchukua Nani, mwenye Miaka 29, baada ya kushinda majaribio ya Klabu ya England Stoke City iliyomtaka Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United na Sporting Lisbon.

Nani, ambae ameifungia Portugal Bao 20 katika Gemu 101, aliichezea Fenerbahce Mechi za Ligi 28 Msimu uliopita na kufunga Bao 20.
Akiwa na Man United, Nani alishinda Mataji ya Ubingwa wa England Manne katika Miaka yake Minane huko Old Trafford na kuhamia Fenerbahce Msimu uliopita baaada ya kukaa kwa Mkopo huko Sporting Lisbon Msimu wa 2014/15.