Friday, July 1, 2016

NEYMAR ASAINI MKTABA MPYA BARCELONA

Neymar amesaini Mkataba mpya na Barcelona ambao utambakisha hapo hadi Juni 2021
Na una kipengele cha Klabu kulipwa Pauni Milioni 210 ikiwa atatakiwa na Klabu nyingine wakati huu wa Mkataba wake.
Neymar, ambae alibakisha Miaka Miwili kwenye Mkataba wake uliopita, amekuwa akiripotiwa kutakiwa na Klabu nyingine ambazo zilitajwa kuwa ni PSG na Manchester United.
Lakini sasa hayo yatanyamazishwa kwa Mkataba huu mpya wenye kipengele cha Barca kulipwa Pauni Milioni 167 ikiwa atatakiwa na Klabu nyingine ndani ya Mwaka Mmoja wa wa Mkataba wake huu na Dau hilo kupanda hadi Pauni Milioni 185 kwa Mwaka wa Pili wa Mkataba na kufikia Pauni Milioni 210 kwa Miaka Mitatu iliyobaki ya Mkataba.

Neymar, ambae sasa amemaliza Miaka Mitatu akiwa na Barca, Msimu wa 2015/16 uliokwisha Mei alifunga Goli 31 katika Mechi 49 na kuisadia Barca kutwaa Ubingwa wa La Liga na Copa del Rey.
Katika Mechi 141 alizoichezea Barca hadi sasa, Neymar amepachika Mabao 85.
eymar, ambae hakuichezea Brazil kwenye Copa America Centenario huko USA Mwezi uliopita, akipumzishwa ili aichezee Brazil kwenye Michezo ya Olimpiki itakayofanyika huko Brazil Mwezi Agosti.