Thursday, July 21, 2016

POGBA ANARUDI... OLD TRAFFORD, JUVE WAKUBALI YAISHE!


Habari hizi za Sky Sports zimetoboa kuwa kilifanyika Kikao cha pamoja
Kati ya Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Man United, Ed Woodward, Wakala wa Pogba, Mino Raiola, na Meneja Mkuu wa Juventus, Giuseppe Marotta huku Pogba mwenyewe akiwa bado vakesheni na anatarajiwa kuingia mazoezini hapo Agosti 6.
Akiwa na Juve, Pogba ameweza kutwaa Ubingwa wa Serie A mara 4 na Coppa Italia 2.
Wakati alipotambulishwa rasmi kama Meneja Mpya wa Man United, Jose Mourinho, alidokeza kuwa nia na la muhimu kwake ni kusaini Wachezaji Wanne katika kipindi hiki cha Uhamisho na tayari amesaini Watatu ambao ni Eric Bailly, Henrikh Mkhitaryan na Zlatan Ibrahimovic.

Jana Man United walisafiri kwenda huko China kufanya Ziara ya kabla Msimu mpya kuanza ambako watacheza Mechi 2 za Kirafiki dhidi ya Borussia Dortmund na Manchester City.
Kwenye Kikosi cha Wachezaji 25 waliosafiri wapo wapya Mkhitaryan na Bailly lakini Ibrahimovic bado yupo mapumzikoni.

Pogba played for Manchester United as a youngster but left to join Juventus on a free transfer in 2012KIKOSI KAMILI KILICHOSAFIRI:
De Gea, Romero, Johnstone, Bailly, Blind, Fosu-Mensah, Jones, McNair, Rojo, Shaw, Smalling, Tuanzebe, Valencia, Carrick, Herrera, Januzaj, Lingard, Mata, Memphis, Mkhitaryan, A. Pereira, Young, Keane, Rashford, Rooney.
Ratiba/Matokeo:
Julai 2016
16 Jul Kirafiki: Wigan Athletic 2 - 0
22 Jul Ziara 2016: Borussia Dortmund [China, Saa 9 Mchana]
25 Jul Ziara 2016: Manchester City [China, Saa 8 na Nusu Mchana]
30 Jul Ziara 2016: Galatasaray [Sweden, Saa 2 na Nusu Usiku]
Agosti 2016
03 Aug Wayne Rooney Mechi Maalum: Everton [Old Trafford, Saa 4 Usiku]
07 Aug FA Community Shield: Leicester City [Wembley, Saa 12 Jioni]
Ligi Kuu England
14 Aug: Bournemouth [Ugenini, Saa 9 na Nusu Mchana]
19 Aug: Southampton [Old Trafford, Saa 4 Usiku]
27 Aug: Hull City [Ugenini, Saa 1 na Nusu Usiku]
Septemba 2016
10 Sep: Manchester City [Old Trafford, Saa 8 na Nusu Mchana]
18 Sep: Watford [Ugenini, Saa 8 Mchana]
24 Sep Premier League Leicester City [Old Trafford, Saa 8 na Nusu Mchana]