Tuesday, July 5, 2016

POGBA ANATAKIWA NA MAN UNITED, LICHA WAKALA WAKE KUWA NA BIFU NA SIR ALEX FERGUSON!

ZIPO ripoti thabiti kuwa Kiungo wa Klabu ya Juventus na ambae sasa anaichezea Timu ya Taifa ya France ambayo ipo Nusu Fainali ya EURO 2016, Paul Pogba, anatakiwa na Manchester United licha ya Meneja Lejendari wa Klabu hiyo, Sir Alex Ferguson kudai hampendi Wakala wa Mchezaji huyo.
Pogba aliondoka Man United Mwaka 2012 baada ya kuugomea Mkataba Mpya na kwenda Juventus na wakati huo aliekuwa Meneja wa Man United Sir Alex Ferguson kusema alitaka Kijana huyo abaki lakini Wakala wake, Mino Raiola, alikuwa ‘sumu’.

Akiandika kwenye Kitabu cha Maisha yake, ‘Leading’, Sir Alex Ferguson alisema: “Wapo Mawakala Wawili au Watatu wa Soka ambao siwapendi na mmoja wao ni Mino Raiola, Wakala wa Paul Pogba!”

“Sikumwamini tangu Siku ya kwanza niliyokutana nae. Tulikuwa na Pogba kwa Mkataba wa Miaka Mitatu uliokuwa na Kipengele cha Nyongeza ya Mwaka Mmoja. Ghafla Raiola akaingia na Mkutano wetu wa kwanza ulikuwa balaa!”

“Yeye na mimi tulikuwa kama maji na mafuta. Na yeye akawarubuni Familia ya Kijana huyo na akasaini Juve!”

Lakini hivi sasa, Wachambuzi wanasema kuwa uhusiano wa Ferguson na Raiola si kikwazo tena kwa Pogba kujiunga Man United.
Tayari Raiola, ambae ni Wakala wa Mastaa Wawili Zlatan Ibrahimovic na Henrikh Mkhitaryan, ameshasuka Wachezaji hao kutua Man United.
Lakini huenda Dau la kumnunua Pogba, Karibu Euro Milioni 100, likawa kikwazo kwa Mchezaji alieondoka bure bila kulipwa Senti.