Friday, July 8, 2016

POGBA KUWAAGA JUVENTUS KURUDI MAN UNITED WALIOMWEKEA PESA YA REKODI MEZANI £106m


Paul Pogba ameonyesha nia yake kukamilisha kurejea tena Manchester United kwa mujibu wa ripoti kutoka Ufaransa.
Jarida maarufu huko France, L'Equipe, limedai Pogba amewaambia Marafiki zake na Wachezaji wenzake kwamba anataka kurejea Man United ikiwa ni Miaka Minne tangu aondoke Old Trafford kwenda kujiunga na Klabu ya Italy Juventus.
Mino Raiola, Wakala wa Pogba, amepewa jukumu la kutoa Ofa kwa Juventus ili Mchezaji huyo ajiunge na Man United mara tu baada ya Fainali za EURO 2016 kumalizika.

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2016/07/07/16/360A690200000578-0-image-a-23_1467906493290.jpgInasemekana Meneja mpya wa Man United, Jose Mourinho, anamtaka Pogba ajiunge na Kikosi chake kabla ya Mechi yao ya kufungua pazia Msimu Mpya kugombea Ngao ya Jamii hapo Agosti 7 dhidi ya Leicester City Uwanjani Wembley Jijini London.
Kwa mujibu wa L'Equipe, Raiola alikutana na Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Man United Ed Woodward huko France hapo Jana kujadili Dili hii.
Klabu ya Pogba, Juventus, inataka ilipwe si chini ya Pauni Milioni 90 ambayo ni Rekodi ya Dunia ili imwachie Mchezaji huyo alieondoka Man United bila kulipwa Senti na Dau hilo linasemwa si kikwazo kwa Klabu hiyo.
http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2016/07/06/21/11D877A000000514-3677723-image-a-2_1467835904920.jpg