Saturday, July 30, 2016

POGBA NDANI YA OLD TRAFFORD, AFUZU ‘AFYA’, KUZOA MKWANJA MREFU

IMEVUJA kwamba Paul Pogba amefuzu upimwaji afya huko Los Angeles Marekani akiwa njiani kukamilisha Uhamisho wake kutoka Juventus ya Italy kwenda Manchester United ya England.
Pogba, Kijana wa Miaka 23 wa Ufaransa, yuko huko Marekani kwa maumziko na sasa yuko mbioni kuwa Mchezaji alievunja Rekodi ya Dunia kwa Dau la kuuzwa ambalo linaaminika litafika Pauni Milioni 112 na kupiku lile la Gareth Bale alienunuliwa na Real Madrid kutoka Tottenham kwa Pauni Milioni 85 Mwaka 2013.
Akiwa Man United kwa Mkataba wa Miaka Mitano, Pogba atazoa mshahara wa Pauni 275,000 kwa Wiki na kuwa Nambari Wani kwa Mkwanja mzuri.
Akitua Old Trafford, Pogba atakuwa Mchezaji wa 4 mkubwa kununuliwa na Meneja Mpya Jose Mourinho katika kipindi hiki.
Wengine ni Zlatan Ibrahimovic, Eric Bailly na Henrikh Mkhitaryan.

MAN UNITED – WACHEZAJI:
MISHAHARA KWA WIKI:
Pauni 1 ni takriban Shilingi 2880

1 Paul Pogba - £275,000
2 Wayne Rooney - £260,000
3 Zlatan Ibrahimovic - £250,000
4 Henrikh Mkhitaryan - £200,000
4 Bastian Schweinsteiger - £200,000
4 David De Gea - £200,000
7 Juan Mata - £140,000
8 Ashley Young - £110,000
9 Morgan Schneiderlin - £100,000
10 Memphis - £90,000
11 Marouane Fellaini - £80,000
11 Chris Smalling - £80,000
11 Michael Carrick - £80,000
14 Daley Blind - £75,000
14 Ander Herrera - £75,000
14 Eric Bailly - £75,000
17 Marcos Rojo - £70,000
17 Antonio Valencia - £70,000
17 Luke Shaw - £70,000
20 Anthony Martial - £65,000
21 Matteo Darmian - £60,000
22 Sergio Romero - £50,000
22 Phil Jones - £50,000
22 Jesse Lingard - £50,000
25 Adnan Januzaj - £40,000
26 Paddy McNair - £25,000
27 Marcus Rashford - £20,000
27 Tyler Blackett - £20,000
29 Cameron Borthwick-Jackson - £10,000
30 Andreas Pereira - £6,000
31 James Wilson - £5,000
31 Will Keane - £5,000
33 Regan Poole - £1,300
MENEJA: Jose Mourinho - £312,500