Thursday, July 28, 2016

RAIS BARACK OBAMA AWATAKA WAPIGA KURA WA MAREKANI KUMCHANGUA BI. CLINTON


Rais wa Marekani Barack Obama amewasihi wapiga kura kuendelea kumuunga mkono kwa kufanikisha Bi. Hillary Clinton kushinda katika uchaguzi mkuu wa rais Novemba.

Obama amemsifia Bi. Clinton katika mkutano wa taifa wa chama cha Democratic huko Philadelphia, kwa kusema ni mtu mwenye sifa zaidi kuwahi kugombea kuingia Ikulu ya Marekani.

Amewaambia wapiga kura kuwa wanakabiliwa na chaguo baina ya matumaini ama hofu na mashambulizi yanayojengwa na mgombea wa Republican Donald Trump.


Rais Barack Obama akikumbatiana na Bi. Hillary Clinton baada ya kumaliza hotuba yake

Bi. Clinton akiwa na furaha tele akiwapungia mkono wajumbe wa Democratic akiwa na rais Barack Obama

Rais Barack Obama akimyanyua mkono juu Bi. Hillary Clinton huku akiwapungia mkono wajumbe wa chama cha Democratic