Friday, July 1, 2016

SASA NI RASMI NOLITO ATUA MAN CITY, NI WA 3 KUSAINIWA NA PEP GUARDIOLA!

Manchester City imemsaini Fowadi wa Spain Nolito kutoka Celta Vigo baada ya kuafiki kulipa Dau la Pauni Milioni 13.8 kama Mkataba wake unavyosema.
Nolito, mwenye Miaka 29 na ambae Jina lake kamili ni Manuel Agudo Duran, amesaini Mkataba wa Miaka Minne na sasa anakuwa Mchezaji wa Tatu kusainiwa na Meneja mpya Pep Guardiola katika kipindi hiki.
Wachezaji ambao Man City tayari imewasaini ni Ilkay Gundogan kutoka Borussia Dortmund na Kiungo wa Australia Aaron Mooy.

Nolito alikuwa huko France akiichezea Timu ya Taifa ya Spain kwenye EURO 2016 na alianza Mechi zao zote 4 hadi walipotupwa nje na Italy baada ya kufungwa 2-0 na Italy kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Akiongea baada ya kumalisha Uhamisho huu, Nolito alisema: “Nadhani Pep Guardiola ni mmoja wa Mameneja Bora Duniani. Anafahamu mengi kuhusu Gemu hii na atanisaidia kuendelea kama Mchezaji.”