Saturday, July 2, 2016

SASA RASMI: MANCHESTER UNITED YAMSAINI ZLATAN IBRAHIMOVIĆ

Manchester United imetangaza rasmi kumsaini Mchezaji wa Kimataifa wa Sweden Zlatan Ibrahimović.
Ibrahimović, mwenye Miaka 34, aliichezea Paris Saint-Germain ya France Mechi 180 na kufunga Mabao 156 na pia ameweza kutwaa Ubingwa katika Nchi 4 tofauti tangu aanze kucheza Soka Mwaka 1999 huko Malmo, Sweden.
Ibrahimovic ameichezea Timu ya Taifa ya Sweden mara 116 nza kufunga Bao 62 hadi alipostaafu Wiki iliyopita.

Akiongea baada ya kusaini Mkataba, Ibrahimovic alisema: “Nimefurahi mno kujiunga na Manchester United na ninangojea kwa hamu kucheza Ligi Kuu England. Pia ninahamu kubwa kufanya kazi tena na Jose Mourinho. Ni Meneja Bora na nipo tayari kwenye hii changamoto mpya nay a kuvutia. Nimefurahia sana maisha yangu ya Soka na sasa nipo tayari kuweka kumbukumbu nzuri England.”

Nae Jose Mourinho alisema: “Zlatan hahitaji utambulisho wowote. Takwimu zinaongea zenyewe. Ibra ni mmoja wa Mastraika Bora Duniani na ni Mchezaji anaejituma Asilimia 100. Ameshinda Ligi muhimu katika Soka la Dunia na sasa ana nafasi kucheza kwenye Ligi Bora Duniani na atasaidia kuisaidia Timu kutwaa Mataji. Nina hakika kipaji chake kitafurahisha Mashabiki Old Trafford na uzoefu wake utasaidia sana Wachezaji wetu chipukizi.”