Friday, July 1, 2016

SIMBA WAMPOKEA UWANJA WA NDEGE KOCHA WAO MPYA JOSEPH OMOG!

KIGOGO WA Soka Tanzania, Simba, Jana Usiku walimpokea Kocha wao mpya Joseph Omog akitokea kwao Cameroon na kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, JNIA, Jijini Dar es Salaam.
Omog, ambae aliwahi kuwa Kocha wa Azam FC kwa Miezi 14, alipokelewa na Katibu mpya wa Simba, Patrick Kahemele.
Leo Simba inatarajiwa kumtambulisha rasmi.
Omog, mwenye Miaka 44 na ambae aliwahi kubeba CAF Confederation Cup Mwaka 2012 akiiongoza AC Leopard ya Congo Brazaville, aliifundisha Azam FC kuanzia Desemba 2013 na kutimuliwa Machi 2015 baada ya kutolewa nje ya CAF CHAMPIONS LIGI na El-Merreikh kwa kufungwa 3-0 huko Sudan ingawa walishinda Mechi ya Kwanza Dar es Salaam Bao 2-0.

Omog, ambae alitwaa mikoba kutoka kwa Stewart Hall, aliweza kuipa Azam FC Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Mwaka 2014 bila kufungwa hata Mechi moja na katika kipindi chake hicho cha Miezi 14 alisimamia Mechi 55 na Kushinda 30, Sare 14 na kufungwa 11.