Monday, July 4, 2016

SIMBA YAMTAMBULISHA RASMI KOCHA WAKE MPYA, JOSEPH OMOG KUTOKA CAMEROON

RAIS wa Simba, Evans Aveva akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo
KATIBU Mkuu wa Simba, Patrick Kalemela akizungumza
OMOG naye alipata nafasi ya kusema yake ya moyoni wakati wa mkutano huo
KLABU ya Simba jana ilimtambulisha rasmi kocha wake mpya, Joseph Omog kutoka Cameroon.
Omog, ambaye aliwahi kuifundisha Azam msimu uliopita kabla ya mkataba wake kukatishwa, ameingia mkataba wa kuifundisha Simba kwa miaka miwili.
Kocha huyo kutoka Cameroon, anachukua nafasi ya kocha wa zamani wa timu hiyo, Jackson Mayanja kutoka Uganda.

Akizungumza katika mkutano huo, Rais wa Simba, Evans Aveva alisema wameamua kumpa Omog mkataba wa mwaka mmoja kwa ajili ya majaribio. Alisema iwapo atafanya vizuri, wanaweza kumuongezea mkataba mwingine.


Kwa mujibu wa Aveva, kocha huyo amepewa nafasi ya kuchagua wasaidizi wake wa benchi la ufundi na kusisitiza kwamba, uongozi hautamuingilia.
Kwa upande wake, Omog alisema amefurahi kurudi tena Tanzania na kuahidi kufanya kila linalowezekana kuiletea Simba mafanikio.