Tuesday, July 26, 2016

STOKE CITY YAJIPANGA KUNUNUA WACHEZAJI WAWILI KUTOKA LIVERPOOL KWA MPIGO! MAJOGOO SASA WAFIKISHA 7 KUUZA!

STOKE City wapo mbioni kunyakua Wachezaji Wawili kwa mpigo. Kiungo wa Liverpool Joe Allen Leo anatarajiwa kupimwa Afya huko Stoke City ili kukamilisha Uhamisho wa Dau la Pauni Milioni 13 wakati Winga Chipukizi kutoka Al Ahly Ramadan Sobhi akithibitishwa kusainiwa na Meneja wa Stoke Mark Hughes.

Joe Allen
Kiungo wa Wales Joe Allen yupo mbioni kuhama baada ya Klabu yake Liverpool kukubali Ofa ya Stoke City.

Allen, mwenye Miaka 26 na ambae amebakiza Mwaka Mmoja tu kwenye Mkataba wake na Liverpool, alianza Mechi 8 tu huko Anfield Msimu uliopita lakini bado akaitwa kuichezea Timu ya Taifa ya Wales kwenye EURO 2016 na kung’ara mno kiasi cha UEFA kumteua kuwa mmoja wa wa Wachezaji wa Kikosi Bora cha Fainali za EURO 2016.

Ramadan Sobhi
Imethibitika kuwa Stoke City imemsaini Winga wa Misri Ramadan Sobhi kutoka Al Ahly kwa Dau ambalo linaweza kufikia Pauni Milioni 5.

Sobhi, mwenye Miaka 19, alianza kucheza Soka kwenye Timu ya Kwanza ya Al Ahly akiwa na Miaka 16 na sasa kuichezea Mechi 71 Timu hiyo na kutwaa Ubingwa wa Misri mara mbili.