Saturday, July 30, 2016

TEMEKE MARKET YATWAA UBINGWA WA NDONDO CUP

FAINALI ya Sports Extra Ndondo Cup imemalizika leo Jumamosi Julai 30, 2016 kwa timu ya Temeke Market kuibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Kauzu FC mchezo uliopigwa katika dimba la Uwanja wa Bandari (Wembly), Jijini Dar es salaam. Mchezo huo umeshuhudia timu ya Temeke Market ikiibuka mabingwa kwa kuwafunga Kauzu FC ambapo Mabao ya Temeke Market yalifungwa na Ramadhan Madebe, Shaban Kisiga na Adam Kingwande huku lile la Kauzu FC likifungwa na Rashid Tumbo.