Thursday, July 28, 2016

TETESI KUTOKA OLD TRAFFORD: MOURINHO KUWAMWAGA 9 AKIWEMO SCHWEINSTEIGER!

MASHABIKI WAMCHARUKIA KUHUSU FOSU-MENSAH!
KEPTENI wa Mabingwa wa Dunia Germany Bastian Schweinsteiger ni miongoni mwa Wachezaji 9 ambao wanadaiwa kuambiwa na Meneja wa Manchester United Jose Mourinho kwamba hawapo kwenye mipango yake kwa ajili ya Msimu mpya.

Wachezaji hao 9 waliarifiwa uso kwa uso na Mourinho na hii Leo hawakufanya Mazoezi na Kikosi cha Kwanza cha Man United ambacho kilikuwa na Staa mpya Zlatan Ibrahimovic kwa mara ya kwanza na badala yake wote 9 kujumuika na Timu ya U-21.
Inaaminika 9 hao hawatakuwemo kwenye Kikosi cha Man United ambacho kitasafiri kwenda Gothenburg, Sweden na kucheza Jumamosi na Galatasaray.
Mourinho alishaelekeza kuwa anataka kupunguza Kikosi chake kuwa na Wachezaji 24 tu.

Miongoni mwa watakaokatwa ni Chipukizi Cameron Borthwick-Jackson na Tim Fosu-Mensah, ambao Msimu uliopta waling’ara chini ya Louis van Gaal, na mwingine ni Kiungo wa Timu ya Taifa ya Brazil ya U-21 Andreas Pereira ambae atapelekwa nje kwa Mkopo ilia pate uzoefu pamoja na Straika James Wilson.

Wengine ambao watatupwa nje ni Adnan Januzaj, Will Keane, Tyler Blackett na Paddy McNair. Lakini Jina la Tim Fosu-Mensah, mwenye Miaka 18, kuwemo kwenye Listi hiyo ya wanaotemwa kumeibua hisia kali za Mashabiki wa Man United kwenye Mitandao wakidai huyo ni jembe na abakishwe kwa njia yeyote ile.  

9 AMBAO HAWAKO KWENYE MIPANGO YA MOURINHO:
MABEKI:
Tim Fosu-Mensah, Paddy McNair, Tyler Blackett, Cameron Borthwick-Jackson.
VIUNGO: Bastian Schweinsteiger, Andreas Pereira, Adnan Januzaj
MASTRAIKA: Will Keane, James Wilson