Sunday, July 17, 2016

TUZO ZA VODACOM 2015/2016 ZAFANYIKA LEO HII USIKU! JUMA ABDUL MCHEZAJI BORA!

USIKU huu huko Hoteli ya Double Tree Jijini Dar es Salaam imefanyika Hafla ya kutunuka Tuzo za Ligi Kuu Vodacom kwa Msimu wa 2015/16 ambao Yanga waliibuka ni Mabingwa na kama ilivyotarajiwa Klabu hiyo imezoa Tuzo zote kubwa za Mchezaji Bora, Kocha Bora, Mchezaji Bora kwa Wageni na Mfungaji Bora.


WASHINDI WA TUZO:
-MCHEZAJI BORA: Juma Abdul [Yanga]
-MCHEZAJI BORA WAGENI: Thaban Kamusoko [Yanga]
-MFUNGAJI BORA: Amissi Tambwe [Yanga]
-KOCHA BORA: Hans van Pluijm [Yanga]


Wengineo:
-Mwamuzi Bora: Ngole Mwangole
-Kipa Bora: Aishi Manula [Azam FC]
-Goli Bora: Ibrahim Ajib [Simba]
-Mchezaji Bora Chipukizi: Mohammed Hussein [Simba]
-Timu yenye Nidhamu: Mtibwa Sugar


HABARI ZA AWALI:
WANAOWANIA TUZO 13 LIGI KUU YA VODACOM

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limetangaza wanamichezo wote wanaowania tuzo 13 kwenye hafla ya washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2015/2016 itakayofanyika Jumapili (Julai 17 mwaka huu) kwenye hoteli ya Double Tree by Hilton jijini Dar es Salaam.

Aina 13 za tuzo ya Ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania zitatolewa kwa washindi chini ya uratibu wa Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inayoundwa na waandishi wa habari za michezo, makocha, viongozi (administrators) na wawakilishi kutoka kwa wadhamini (Vodacom na Azam Tv).

Tuzo hizo na kiasi cha fedha wanazopata washindi kwenye mabano ni
Bingwa (sh. 81,345,723)
Makamu bingwa (sh. 40,672,861)
3. Mshindi wa Tatu Milioni 29
4. Mshindi wa nne (sh. 23,241,635)
5. Timu yenye Nidhamu Bora (sh. 17,228,820)

*Zilizopendekezwa kuwania tuzo hiyo ni:
- JKT Ruvu
- Mgambo Shooting na
- Mtibwa Sugar

6. Mchezaji Bora wa Ligi (sh. 9,228,820)
*Waliopendekezwa (nominees) kuwania tuzo hiyo ni:
- Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar)
- Juma Abdul (Yanga) na
- Mohamed Hussein (Simba)
7. Mfungaji bora (sh. 5,742,940) 


8. Kipa Bora (sh. 5,742,940)
*Waliopendekezwa (nominees) kuwania tuzo hiyo ni:
- Aishi Manula (Azam),
- Beno Kakolanya (Tanzania Prisons) na
- Deogratius Munishi (Yanga)

9. Mchezaji Bora wa Kigeni (sh. 5,742,940)
- Donald Ngoma (Yanga)
- Thabani Kamusoko (Yanga)
- Vincent Agban (Simba)

10. Kocha Bora (sh. 8,000,000)
*Waliopendekezwa (nominees) kuwania tuzo hiyo ni:
- Hans Van Pluijm (Yanga)
- Mecky Maxime (Mtibwa Sugar) na
- Salum Mayanga (Tanzania Prisons) 


11. Mwamuzi bora (sh. 5,742,940)
*Waliopendekezwa (nominees) kuwania tuzo hiyo ni:
- Anthony Kayombo
- Ngole Mwangole
- Rajab Mrope

12. Mchezaji Bora Chipukizi (sh. 4,000,000

*Waliopendekezwa (nominees) kuwania tuzo hiyo ni:
- Farid Mussa (Azam)
- Mohamed Hussein (Simba)
- Mzamiru Yasin (Mtibwa Sugar) na
- Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar)

13. Goli bora la msimu (sh. 3,000,000)
*Kinyang'anyiro cha goli bora ni:
- Ibrahim Ajib (magoli mawili ) na
- Amisi Tambwe (goli moja)
IMETOLEWA NA TFF