Tuesday, July 19, 2016

UEFA YATANGAZA 10 WA KUGOMBEA TUZO MCHEZAJI BORA WA MSIMU ULIOPITA! MESSI, RONALDO NDANI!

Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wapo kwenye Listi ya Wachezaji 10 wanaowania Tuzo ya UEFA ya Mchezaji Bora wa Ulaya kwa Msimu uliopita wa 2015/16.
Kwenye Listi ya mwanzo iliyopigiwa Kura ili kuchuja kupata hawa 10 alikuwamo Will Grigg aliepata umaarufu wakati wa Fainali za EURO 2016 bila kucheza Mechi na ambae alizoa Kura sawa na Wachezaji maarufu Paul Pogba na Giorgio Chiellini na wote kukamata Nafasi ya 25.
Grigg ni Mchezaji wa Northern Ireland ambae aliimbwa kwenye Wimbo ulioimbwa kwenye EURO 2016-WILL GRIGG ON FIRE-na kupendwa na Mashabiki.
Kwenye Listi hii ya 10 Bora, Ronaldo, ambae ndie Kepteni wa Portugal iliyobeba EURO 2016, yuko pamoja na Pepe ambae pia alikuwa nae kwenye Kikosi cha Portugal na pia wapo Klabu moja Real Madrid ya Spain.
Wachezaji wengine wa Real, ambao ndio Klabu Bingwa ya Ulaya kwenye Listi hiyo Wachezaji 10 ni Gareth Bale na Toni Kroos.
Wachezaji hawa 10 watapigiwa tena Kura toka kwa Wanahabari maalum toka Nchi 55 Wanachama wa UEFA hapo Agosti 5 ili kubakiza 3 Bora ambapo Mshindi atatangazwa Agosti 25 wakati wa Droo ya kupanga Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI huko Monaco.

10 BORA:
-Gareth Bale (Wales, Real Madrid)
-Gianluigi Buffon (Italy, Juventus)
-Antoine Griezmann (France, Atletico Madrid)
-Toni Kroos (Germany, Real Madrid)
-Lionel Messi (Argentina, Barcelona)
-Thomas Mueller (Germany, Bayern Munich)
-Manuel Neuer (Germany, Bayern Munich)
-Pepe (Portugal, Real Madrid)
-Cristiano Ronaldo (Portugal, Real Madrid)
-Luis Suarez (Uruguay, Barcelona).