Thursday, July 7, 2016

UHAMISHO 2016: HENRIKH MKHITARYAN ATUA MAN UNITED.

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2016/07/07/13/360195AC00000578-0-image-a-72_1467894172297.jpgManchester United imetangaza rasmi kuwa Henrikh Mkhitaryan amekamilisha Uhamisho wake kutoka Borussia Dortmund.
Kiungo huyo sasa amesaini Mkataba wa Miaka Minne na Man United ambao una nyongeza ya Mwaka mmoja.
Mkhitaryan, mwenye Miaka 27, aliichezea Dortmund Mechi 140 na kufunga Bao 41 tangu ajiunge nao Mwaka 2013.


Msimu uliopita, Mkhitaryan aliifungia Dortmund Bao 23 na kutengeneza Bao 32 na kuteuliwa kuwa ndie Mchezaji Bora wa Bundesliga kwa Msimu wa 2015/16 na pia kuwemo kwenye Timu ya Msimu iliyoteuliwa na Chama cha kutetea Haki za Wachezaji wa Kulipwa huko Germany, VDV.
Kiungo huyu ndie Mfungaji Bora katika Historia ya Timu ya Taifa ya Armenia akiwa na Bao 19 katika Mechi 59 tangu aanze kuichezea January 2007 na pia ndie Kepteni wa Timu hiyo huku pia akizoa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Armenia kwa mara 5.

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2016/07/07/13/3601930200000578-3678897-image-a-107_1467896219296.jpgAkiongea baada ya kukamilika Uhamisho, Mkhitaryan alisema: “Nasikia fahari mno kujiunga na Manchester United, hili ni ndoto yangu kutimia!”
http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2016/07/07/13/3601951000000578-3678897-Henrikh_Mkhitaryan_became_Jose_Mourinho_s_third_summer_signing_a-a-108_1467896228420.jpgNae Meneja wa Man United, Jose Mourinho, alieleza: “Henrikh ni Mchezaji mwenye Kipaji kikubwa ambae amekuwa kwenye fomu nzuri mno kwa Klabu na Nchi yake. Ni Mchezaji mahiri wa Kitimu mwenye uwezo mkubwa, uelewa na jicho safi la kufunga magoli. Nimefurahio ameichagua United. Naamini ataleta msukumo kwenye Timu kwani uchezaji wake ni sahihi kwa Ligi Kuu.”http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2016/07/07/13/3601930900000578-3678897-Mkhitaryan_has_moved_to_Old_Trafford_for_as_fee_of_26million_fro-a-106_1467896210229.jpg