Saturday, July 30, 2016

UHAMISHO: ATLETICO MADRID WAMNYATIA COSTA DARAJANI

Atletico Madrid Wanataka kumnunua Mchezaji matata wa Chelsea Diego Costa ili kumrudisha kwenye Klabu yake ya Zamani baada ya mambo yake kwenda kombo England.
Atletico Madrid, Timu yake ya zamani, imetoa Dau la Pauni Milioni 40 kumrudisha huko.
Costa yupo Benchi huko Marekani akijiuguza maumivu ya mgongo lakini Conte hakutoa jibu la uhakika alipohojiwa kuhusu Costa kurudi Atletico baada ya kukaa Miaka Miwili na Chelsea.
Conte alieleza: "Naweza kusema Leo Costa ni Mchezaji wa Chelsea. Hakucheza kwa sababu ana maumivu. Akipona anaweza kucheza Jumatano na Milan. Naongea kuhusu Leo na Leo Costa yupo Chelsea. Kesho, ukiniuliza kama Costa atabaki, sijui."
Inaaminika Conte anataka kumrejesha tena Romelu Lukaku kutoka Everton lakini hadi sasa wamegoma hadi Chelsea ilipe Dau la Pauni Milioni 75.
Conte alikataa kumzungumzia Lukaku na kusisitiza haongelei Wachezaji wa Timu nyingine.