Sunday, July 10, 2016

UHAMISHO: GRAZIANO PELLE KUIHAMA SOUTHAMPTON KWENDA CHINA

Graziano Pelle ataihama Southampton na kwenda kucheza huko China kwa Dau la Pauni Milioni 13.
Pelle, ambae atatimiza Miaka 31 Wiki ijayo na ambae aling’ara hivi Juzi huko France akiichezea Italy chini ya Meneja Mpya wa Chelsea Antonio Conte, pia amekuwa akihusishwa na kuhamia Chelsea.
Lakini habari za ndani zimedokeza kuwa Pelle atakwenda kujiunga na Klabu ya China Shandong Luneng.

Uhamisho huu utaifanya Southampton, maarufu kama ‘Watakatifu’, kupata faida ya Pauni Milioni 4 kwa Mchezaji waliemsaini kutoka Feyenoord Miaka Miwili iliyopita.

Katika kipindi hiki, Southampton tayari ishawauza Victor Wanyama kwa Spurs na Sadio Mane kwa Liverpool kwa Dau la Rekodi la Pauni Milioni 36.