Tuesday, July 12, 2016

WEST HAM WAMPANDISHA BEI DIMITRI PAYET, WADAI HAUZWI, ILA THAMANI YAKE NI £100M!

MWENYEKITI MWENZA wa West Ham David Sullivan amesema Dimitri Payet ana thamani ya Pauni Milioni 100 lakini ‘hauzwi’.
Payet, ambae aling’ara akiichezea France kwenye EURO 2016 na kuteuliwa kuwa Mchezaji kwenye Timu Bora ya Fainali hizo, sasa anawindwa na Klabu kubwa za Ulaya.

Akiongea na Gazeti la Uingereza, Daily Mirror, Sullivan alisema: “Payet hauzwi. Thamani yake ni Pauni Milioni 100!”
Lakini Sullivan alisema ikiwa ipo Klabu ambayo iko tayaria kulipa Thamani hiyo basi wao wako tayari kuisikiliza.

Sullivan, ambae pamoja na David Gold, ndio Wamiliki wa West Ham, amesema hawatakubali kuburuzwa na Klabu kubwa ili wamuuze Payet.
Sullivan ameeleza: “Tulimpa Payet Mkataba mpya. Na akiendelea kucheza vizuri mwishoni mwa Mwaka au Msimu tunaweza kumpa Mkatapa mpya mwingine.”

Aliongeza: “Ni Miezi Minne tu iliyopita tulimpa Mkataba mpya na sidhani baada ya Mechi chache na France anastahili Mkataba mpya ikiwa ni Miezi Minne tu!”