Saturday, July 16, 2016

WIGAN 0 vs 2 MAN UNITED, BAILLY, MKHITARYAN WAANZA KUUTAFUTA MSIMU VYEMA KWA MAN UNITED.

USHINDI mzuri wa Bao 2-0 umeashiria mwanzo mwema kwa Manchester United chini ya Meneja mpya Jose Mourinho.
Wakicheza kwao DW Stadium, Wigan Athletic, inayocheza Daraja la Championship, ilishindwa kufurukuta na kujikuta ikichapwa 2-0 kwa Bao za Kipindi cha Pili za Will Keane na Andreas Pereira ziluzofungwa Dakika za 49 na 58.
Wachezaji wapya wa Man United, Henrikh Mkhitaryan na Eric Bailly walianza Mechi hii na kucheza vizuri wakati Luke Shaw ambae alikuwa nje kwa Miezi 10 baada ya kuvunjika Mguu mara 2 alijitahidi sana.
Baada ya kuwa Sare 0-0 hadi Mapumziko, Mourinho alibadili Wachezaji 7 wakati wa Mapumziko kwa kuwaingiza Jones, Mata, Januzaj, Pereira, Young, Valencia na Keane kwabadili Fosu-Mensah, Shaw, Carrick, Lingard, Mkhitaryan, Memphis na Wilson. Jose Mourinho
Katika Dakika ya 74, Manchester United waliwabadili Blind na Herrera na kuwaingiza Gulliermo Varela and Tyler Blackett.