Monday, July 18, 2016

YANGA WASHINDWA KUTAMBA NYUMBANI, WATOKA SARE YA 1-1 NA MEDEAMA


Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akimtoka kipa wa Medeama, Daniel Agyei na kuipatia timu yake goli katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilitoa sare ya 1-1. (Picha na Francis Dande)

Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa akimtoka beki wa Medeama ya Ghana katika mchezo wa Kombe la Shirikisho.

Amisi Tambwe akiwatoka mabeki wa Medeama.

Wachezaji wa Yanga wakitoka uwanja huku wakiwa vicxhwa chini baada ya kutoka sare ya 1-1 na Medeama.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga aliyefungiwa kwa kipindi cha mwaka mmoja kutojihusisha na masuala ya soka, Jerry Muro 'aliyeshika bendera', akiwaongoza mashabiki wa hiyo

Wanayanga wakiishangilia timu yao.

Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akishangilia bao aliloifungia timu yake kabla ya Medeama kusawazisha.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia.

Kiungo wa Medeame, Abbas Mohamed akiwashukuru mashabiki wa Simba kwa kuisapoti timu hiyo mara baada ya mchezo kumalizika.

Wachezaji wa timu ya Medeame wakifurahia sare ya 1-1 baada ya kumalizika kwa mechi yao na Yanga.

Waziri wa mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akifurahia jambo na Kocha wa Mwadui FC, Jamhuru Kihwelu 'Julio' walipokutana Uwanja wa Taifa wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho.

Mashabiki wa Yanga.

Beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro' (kulia), akiwa na mshambuliaji wa timu hiyo, Haruna niyonzima kabla ya kuanza kwa mchezo.
Waamuzi wakiingia uwanjani.
Mashabiki wa Yanga wakiisapoti timu yao.
Waamuzi wa mchezo huo wakiwa katika picha ya pamoja na manahodha wa timu zote.
Kikosi cha Yanga.