Friday, July 1, 2016

ZLATAN IBRAHIMOVIC ATHIBITISHA KUJIUNGA MANCHESTER UNITED

LEO Zlatan Ibrahimovic amethibitisha yeye mwenyewe kwamba anajiunga na Manchester United.
Ibrahimovic aliposti kwenye Instagram ujumbe ambao ulisomeka: “Ni wakati wa kuijulisha Dunia. Ninakokwenda ni Manchester United #iamcoming.”
Lakini habari za ndani za Man United zimedokeza kuwa hamna dili iliyosainiwa na Mchezaji huyo, mwenye Miaka 34, anapaswa kwanza kupimwa afya yake Wiki ijayo.
Ikiwa Ibrahimovic atatua Old Trafford ataungana na Jose Mourinho ambae walikuwa wote huko Italy Kilabuni Inter Milan na kuwa na ushirika wazuri.
Ibrahimovic atakuwa Mchezaji wa pili kujiunga na Man United baada ya kusainiwa Eric Bailly na pia njiani yupo Kiungo wa Borussia Dortmuna, Henrikh Mkhitaryan, ambae Dau lake limeshaafikiwa na Klabu hizo mbili.

Habari hizi za kujiunga kwa Ibrahimovic na Man United zimekuja Saa chache tu baada ya Man United kuthibitisha kucheza Mechi ya Kirafiki na Galatasaray ya Uturuki huko Gothenburg, Sweden hapo Julai 30 na hiyo ni nafasi murua kwa Mashabiki wa Nchi hiyo kuonyesha shukran zao kwa Staa wao Ibrahimovic ambae Wiki iliyopita alistaafu kuichezea Nchi hiyo ambayo yeye ndie Mfungaji Bora katika Historia yao.