Tuesday, August 16, 2016

2016/17 UEFA CHAMPIONS LEAGUE, STEAUA BUCURESTI 0 v 5 MANCHESTER CITY


WAKICHEZA Ugenini huko Steau Stadium, Bucharest Nchini Romania katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mwisho ya Mchujo ya UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, Manchester City wameifumua Steau Bucharest 5-0 na kujiweka pazuri mno kusonga Wiki ijayo katika Mechi ya Marudiano.
Licha ya Sergio Aguero kukosa Penati 2 katika Mechi hii, moja ikiokolewa na Kipa na nyingine kupaa juu, Muargentina huyo alijirekebisha na kupiga Hetitriki.
Bao nyingine za City zilifungwa na Nolito na David Silva.

City watarudiana na Steau Jumatano ijayo huko Etihad Stadium Jijini Manchester na Mshindi kutumbukizwa kwenye Droo ya kupanga Makundi itakayofanyika Agosti 25.

David Silva dakika ya (13') anaipachikia bao la kuongoza Man City sasa ni 1-0 dhidi ya Steaua Bucuresti.