Thursday, August 18, 2016

ARSENE WENGER ASEMA KLABU IPO TAYARI KUTUMIA FEDHA KUNUNUA WAPYA!

Arsene Wenger amesisitiza yuko tayari kutumia Fedha kununua Wachezaji wapya kabla Dirisha la Uhamisho halijafungwa Agosti 31.
Hadi sasa, katika kipindi hiki cha Uhamisho kilichoanza rasmi Julai Mosi, Arsenal imeshagomewa na Jamie Vardy wa Mabingwa wa England Leicester City wakati Ofa yao kumnunua Straika wa Lyon Alexandre Lacazette imegomewa na Klabu hiyo ya France na pia nia yao kumchukua Sentahafu wa Valencia ya Spain Shkodran Mustafi imegota mwamba.
Matukio hayo yamewafanya Mashabiki wa Arsenal kuamini Wenger na Klabu hawana nia kutumia Fedha ikibidi.

Akihojiwa nini kinajiri kuhusu Mustafi, Wenger alijibu: “Naamini ni bora tusizungumzie kuhusu Wachezaji binafsi lakini sisi tunafanya kazi kwa bidii. Nyie mnaamini kabisa kuwa sipo tayari kutumia Fedha lakini nakuhakikishia tupo tayari kutumia Fedha!”