Tuesday, August 30, 2016

BIG SAM ATANGAZA KIKOSI CHAKE CHA KWANZA ENGLAND, ANTONIO WA WEST HAM NDANI!

WINGA wa West Ham Michail Antonio ameitwa kwenye kikosi cha England kwa mara ya kwanza kabisa na Meneja Mpya Sam Allardyce ambae alitangaza Kikosi chake kwa mara ya kwanza.
Pia yumo Fulbeki wa Manchester United Luke Shaw ambae ameitwa kwa mara ya kwanza tangu avunjike Mguu mara 2 Septemba Mwaka Jana akiungana na wenzake wa Man United Kepteni Wayne Rooney na Chris Smalling Kikosini.

England watacheza Mechi yao ya kwanza chini ya Sam Allardyce hapo Septemba 4 Ugenini na Slovakia ikiwa ni Mechi ya Kundi F la Kanda ya Ulaya kuwania kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.

Wengine ambao wamo Kikosini ni Mchezaji wa Arsenal Theo Walcott na yule wa Leicester Danny Drinkwater ambao hawakuwemo Kikosi cha England kilichocheza Fainali za EURO 2016 Mwezi Juni.

Kuhusu muteua Antonio, Allardyce, maarufu kama Big Sam, alisema: “Yupo kwenye Fomu nzuri. Amekuwa na safari ndefu yenye manufaa kutoka Klabu si za Ligi na sasa yupo Timu ya Taifa. Alifunga Bao 9 Msimu wake wa kwanza na ni Mwanamichezo mzuri, ana krosi safi na ni Mfungaji!”

Antonio, aliejiunga na West Ham akitokea Nottingham Forest Septemba 2015, alianzia Soka lake akichezea Klabu zisizokuwa za Ligi Tooting na Mitcham United.

ENGLAND – Kikosi kamili:
Makipa:
Fraser Forster (Southampton), Joe Hart (Manchester City), Tom Heaton (Burnley).
Mabeki: Gary Cahill (Chelsea), Nathaniel Clyne (Liverpool), Phil Jagielka (Everton), Danny Rose (Tottenham Hotspur), Luke Shaw (Manchester United), Chris Smalling (Manchester United), John Stones (Manchester City), Kyle Walker (Tottenham Hotspur).

Viungo: Dele Alli (Tottenham Hotspur), Michail Antonio (West Ham United), Eric Dier (Tottenham Hotspur), Danny Drinkwater (Leicester City), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), Wayne Rooney (Manchester United), Raheem Sterling (Manchester City), Theo Walcott (Arsenal).

Mastraika:
Harry Kane (Tottenham Hotspur), Daniel Sturridge (Liverpool), Jamie Vardy (Leicester City).

England – Ratiba yao:
Septemba 2016
Kombe la Dunia-Kundi F:

Slovakia v England Jumapili Sep 4 1900

Oktoba 2016
Kombe la Dunia-Kundi F:
England v Malta Jumamosi Okt 8 1900

Kombe la Dunia-Kundi F:
Slovenia v England Jumanne Okt 11 2145

Novemba 2016
Kombe la Dunia-Kundi F:

England v Scotland Ijumaa Nov 11 2245
Kimataifa Kirafiki
England v Spain Jumanne Nov 15 2300