Tuesday, August 2, 2016

EDGARDO BAUZA MENEJA MPYA WA ARGENTINA

Chama cha soka cha Argentina (AFA) kimemteua kocha Edgardo Bauza kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa.

Kocha huyu anachukua nafasi iliyoachwa na Gerardo "Tata" Martino aliyejiuzulu baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la Copa America.

AFA walimtangaza kocha huyo baada ya klabu ya Sao Paulo kukubali kumuachia kocha huyo kwenda kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Argentina.

Bauza, mwenye umri wa miaka 58,alikua kocha mkuu mkuu wa klabu ya Sau Paulo toka mwaka 2015 na kuisaidia kufika nusu fainali ya michuano ya Copa Libertadores.
Makocha waliokua wakipewa nafasi ya kukinoa kikosi hicho ni Jorge Sampaoli Marcelo Bielsa.