Tuesday, August 23, 2016

EFL CUP: LEO DIMBANI, CHELSEA, EVERTON, LIVERPOOL NA TIMU KIBAO UWANJANI LEO!

Raundi ya Pili ya EFL CUP, Kombe la Ligi ya England ambalo kwa Miaka Minne lilikuwa likiitwa Capital One Cup kutokana na udhamini wa Capital One, itaanza kuchezwa Leo na Klabu kadhaa za Ligi Kuu England zitaingia dimbani kwa mara ya kwanza.
Msimu huu hili Kombe la Ligi halina Mdhanini na limebatizwa English Football League Cup, EFL CUP.
Miongoni mwa Klabu hizo ni Chelsea, chini ya Meneja mpya Antonio Conte, ambao watacheza kwao Stamford Bridge na Mshindi kati ya Bristol Rovers.
Everton, chini ya Meneja Mpya Ronald Koeman, nao watakuwa kwao Goodison Park kucheza na Klabu ya Ligi 2 Yeovil.
Liverpool wao wapo Ugenini huko Pirelli Stadium kucheza na Timu ya Daraja la Championship Burton.
Klabu za Ligi Kuu England ambazo ziko kwenye Mashindano ya Klabu Ulaya, yale ya UEFA CHAMPIONS LIGI na EUROPA LIGI, zitaanza Raundi ya 3 ya EFL CIP.
Klabu hizo ni Arsenal, Leicester City, Manchester City, Manchester United, Southampton, Tottenham Hotspur na West Ham United.
EFL CUP

RAUNDI YA PILI
Mechi zote Saa 3 Dak 45 Usiku
Jumanne Agosti 23

21:30 Crystal Palace v Blackpool
QPR v Rochdale
Scunthorpe v Bristol City
Watford v Gillingham
Peterborough v Swansea
Everton v Yeovil
Millwall v Nottingham Forest
Luton v Leeds
Chelsea v Bristol Rovers
Burton v Liverpool
Blackburn v Crewe
Preston v Oldham
Oxford v Brighton
Newcastle v Cheltenham
Exeter v Hull
Derby v Carlisle
Northampton v West Brom
Wolves v Cambridge
Stevenage v Stoke
Norwich v Coventry
2200 Reading v MK Dons
Jumatano Agosti 24
Sunderland v Shrewsbury
Accrington v Burnley
Morecambe v Bournemouth
Fulham v Middlesbrough