Monday, August 8, 2016

FULL TIME: MANCHESTER CITY 2 v 3 ARSENAL

Arsenal wamewafunga wenzao wa England Manchester City Bao 3-2 katika Mechi ya Kirafiki iliyochezwa huko Ullevi Stadium, Gothenburg, Sweden.
Mchezaji wa Arsenal Chuba Apkom alionyesha ukali wake kwa kupiga Bao 1 likiwa ni Bao lake la Nne katika Mechi Nne zilizopita.
Timu zote zilishusha Vikosi imara kwenye Mechi hii na City kutangulia kufunga kwa Bao la Sergio Aguero alieunganisha krosi ya Raheem Sterling katika Dakika ya 30.
Alex Iwobi akaisawazishia Arsena Dakika ya 50 na kisha Theo Walcott na Chuba Apkom kuipa Arsenal Bao 3-1 katika Dakika za 73 na 85.

Bao la Pili la City lilifungwa Dakika ya 87 na Kelechi Iheanacho.
Jana Arsenal walipata pigo jingine baada ya Sentahafu wao Gabriel kuumia alipogongana na Raheem Sterling na kulazimika kutolewa kwa Machela.

Arsenal hivi sasa wana pengo kwenye Difensi kufuatia Per Mertesacker kuwa nje kwa muda mrefu kujiuguza Goti.
Kwenye Mechi hii, kila upande uliwatumia Wachezaji kadhaa kwa mara ya kwanza wakitokea Holidei ambapo kwa Arsenal walicheza Alexis Sanchez na Aaron Ramsey na kwa City walikuwepo Aguero na Nolito.