Thursday, August 4, 2016

FULL TIME: Rooney testimonial, MANCHESTER UNITED 0 v 0 EVERTON


Mechi ambayo ilichezwa kwa ajili ya kumtambua na kumuenzi Kepteni wa Manchester United Wayne Rooney iliyochezwa Old Trafford kati ya Man United na Everton ilimalizika kwa Sare ya 0-0.
Rooney aliingia Uwanjani kuanza Mechi hii akiwa na Wanawe Watatu na kuwekewa Gwaride la Wachezaji wa pande zote na kucheza Mechi kwa Dakika 50 na kisha kupumzika kumpisha Marcus Rashford.
Ilitarajiwa Mechi hi ya Timu mbili ambazo ndizo pekee Rooney amezichezea katika maisha yake ya Soka itakuwa laini lakini mara nyingi Wachezaji wa pande zote mbili walijikita kwa Miguu ngangali.
Kipindi cha Pili cha Mechi hii, Meneja wa Man United, Jose Mourinho, akisimamia Mechi yake ya kwanza Uwanjani Old Trafford, alibadili Wachezaji 6 katika Kikosi chake.


VIKOSI:
MAN UNITED:
De Gea (Romero 64), Valencia (Darmian 64), Bailly (Jones 46), Blind (Mata 64), Shaw (Rojo 46), Carrick (Schneiderlin 46), Herrera (Fellaini 46), Lingard (Young 46), Rooney (Rashford 53), Martial (Mkhitaryan 46), Ibrahimovic (Memphis 64)
Akiba Hakutumika: Johnstone.

EVERTON: Stekelenburg (Joel 46), Coleman, Baines (Oviedo 65), Funes Mori, Stones, Holgate (Besic 65 (Davies 77)), McCarthy (Gibson 65), Barry (Cleverley 65), Barkley (Lennon 65), Deulofeu (Mirallas 46), Lukaku (Kone 65)
Akiba Hakutumika: Galloway.