Saturday, August 20, 2016

FULL TIME: STOKE CITY 1 v 4 MANCHESTER CITY

LIGI KUU ENGLAND, EPL, Leo imeanza Raundi ya Pili kwa Mechi ya mapema huko Bitannia Studiam kati ya Wenyeji Stoke City na Manchester City ambayo ilimalizika kwa ushindi wa 4-1 kwa Man City ambao sasa wana Pointi 6 kwa Mechi 2.
City walitangulia kufunga kwa Penati ya Sergio Aguero katika Dakika ya 27 Penati ambayo ilitolewa na Refa Mike Dean baada ya Shawcross kumvuta Otamendi wakati wa Kona.

Aguero aliipeleka City 2-0 kwa Bao la Pili katika Dakika ya 36 baadaya Frikiki ya Kevin de Bruyne kuunganishwa nay eye kwa Kichwa aliporuka juu akiwa kati ya Wachezaji wa Stoke Whelan naWollscheid
Hadi Mapumziko Stoke 0 City 2.

Dakika ya 49 Bojan Krkic, Mchezaji aliewahi kuichezea Barcelona wakati Meneja wa sasa wa City Pep Guardiola yuko huko, aliisawazishia Stoke kwa Penati iliyotolewa baada ya Raheem Sterling kumshika Shawcross wakati wa Kona.

City wajihakikishia Pointi 3 kwa kufunga Bao lao la 3 Dakika ya 85 kupitia Nolito kufuatia kazi njema kati ya De Bruyne, Silva na Iheanacho aliempasia Nolito alieingizwa mwishoni kumbadili Aguero katika Dakika ya 83.
Nolito tena akapiga Bao la 4 Dakika ya 94.