Monday, August 22, 2016

JOEL CAMPBELL AJIUNGA NA SPORTING LISBON YA URENO

Mshambuliaji wa Arsenal Joel Campbel amejiunga na klabu ya Sporting Lisbon nchini Ureno kwa mkopo wa mda mrefu msimu huu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amekuwa na Arsenal tangu mwaka 2011 lakini akashindwa kujiunga na kikosi cha kwanza cha Arsenal.
Alifunga mabao manne katika mechi 30 msimu uliopita,mabao matatu yakitoka kutoka mechi 19 zilizochezwa ugenini.
Campbell ambaye ni raia wa Costa Rica amecheza kwa mkopo katika klabu ya Lorient,Real Betis,Olympiakos na Villareal.

''Kila mtu anamuonbea msimu mzuri huko Ureno'',ilisema taarifa ya mtandao wa Arsenal.
Campbell hajaichezea Arsenal katika mechi mbili za ligi msimu huu.