Friday, August 5, 2016

JOSE MOURINHO: BOSI WA MAN UNITED AFUNGWE KWA ‘KUMYANYASA’ BASTIAN SCHWEINSTEIGER

Mshirika wa FifPro amedai Bosi wa Manchester United Jose Mourinho aswekwe Jela kwa ‘kumyanyasa’ Bastian Schweinsteiger.
Kiungo huyo wa Mabingwa wa Dunia Germany mwenye Miaka 32 alisaini Man United Mwaka Jana kwa Mkataba wa Miaka Mitatu na kucheza Gemu 31 lakini Msimu huu, chini ya Meneja Mpya Jose Mourinho ametupwa kwenye Kikosi cha Rizevu kufanya nao mazoezi. Dejan Stefanovic kutoka Slovenia ambae ni Mwanachama wa FifPro, Chama cha Kutetea Haki za Wachezaji Soka Profeshenali, amedai huo ni ‘unyanyasaji’. Amesema: “Huko Slovenia, tungemshitaki Mourinho na kuomba adhabu ya juu ambayo ni Kifungo cha Miaka Mitatu Jela!’

Stefanovic, ambae ni Mwanasheria na pia ni Rais wa Chama cha Wachezaji Soka na Masapota huko Slovenia, amedai Mourinho anataka kumkatisha tamaa Schweinsteiger.

Schweinsteiger, ambae ni Kepteni wa Timu ya Taifa ya Germany alie aichezea Mechi 120, hajakuwemo kwenye Kikosi cha Kwanza cha Man United kilichocheza Mechi kadhaa za Kirafiki hivi karibuni.

Hilo lilimuudhi hata Ndugu yake aitwae Toby ambae ni Meneja Msaidizi wa U-17 ya Bayern Munich kiasi cha kutinga kwenye  Twitter na kuposti: ‘Hamna Heshima”.

Nae Rais wa Klabu ya zamani ya Schweinsteiger Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge, amesema wachezaji sasa watajiuliza kwanini waende Klabu ya aina hiyo.