Thursday, August 11, 2016

KIRAFIKI: ENGLAND KUCHEZA NA SPAIN WEMBLEY, SAM ALLARDYCE KUONESHA KIKOSI CHAKE!

England watacheza na Spain Mechi ya Kirafiki Uwanjani Wembley Jijini London hapo Novemba 15.
Habari hizi zimetolewa na Chama cha Soka cha England, FA.
Mechi hiyo itakuja Siku 4 tu baada ya England, ambayo iko chini ya Menej mpya Sam Allardyce, kucheza na Scotland katika Mechi ya Kundi lao la kuwania kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za 2018 huko Russia.
Spain nao wataingia kwenye Mechi hiyo wakiwa na Kocha mpya Julen Lopetegui aliembadili Vicente del Bosque alieshindwa kutetea Taji lao kwenye EURO 2016 huko France Mwezi Julai.
Mechi ya England na Spain itakuwa ni Mechi ya 25 kati yao ambapo England wameshinda Mechi 12 kwa 9 za Spain.
Lakini Spain wameshinda Mechi 4 kati ya 5 walizocheza mwisho ikiwemo ile ya mwisho kabisa ambayo Spain walishinda 2-0 huko Alicante, Spain.
Meneja mpya w England Sam Allardyce atasimamia Mechi yake ya kwanza kabisa Mwezi ujao wakicheza na Slovakia katika Mechi yao ya kwanza kabisa ya Kundi lao ya kuwania kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
England
Ratiba

Kombe la Duni -Ulaya- Kundi F
Slovakia v England Jumapili Septemba 4 Saa 1 Usiku

October 2016
Kombe la Duni -Ulaya- Kundi F
England v Malta Jumamosi Oktoba 8 Saa 1 Usiku
Kombe la Duni -Ulaya- Kundi F
Slovenia v England Jumanne Oktoba 11 Saa 2 Dak 45 Usiku

November 2016

Kombe la Duni -Ulaya- Kundi F
England v Scotland Ijumaa Novemba 11 Saa 4 Dak 45 Usiku

Kirafiki
England v Spain Jumanne Novemba 15 Saa 5 Usiku