Wednesday, August 10, 2016

LEO RONALDO, PEPE WAJUMUIKA NA WENZAO MAZOEZINI REAL MADRID.

Cristiano Ronaldo was welcomed back to Real Madrid training by Zinedine ZidaneWACHEZAJI NYOTA wa Mabingwa wa Ulaya Portugal, Cristiano Ronaldo na Pepe, Leo hii wamerejea kwenye Mazoezi ya Klabu yao Real Madrid baada ya kumaliza Likizo yao iliyorefushwa kutokana na ushiriki wao EURO 2016.

Ronaldo na Pepe walicheza Fainali ya EURO 2016 na kuisaidia Portugal kuwabwaga Wenyeji wa Mashindano France na kubeba Ubingwa wa Ulaya hapo Julai 10 Mjini Paris.

Leo walipotua Kambi ya Mazoezi ya Real walikutana na Kocha Zinedine Zidane aliewakaribisha tena Kikosini.

Ingawa Ronaldo amerejea Mazoezini lakini anategemewa asicheze Mechi ya kwanza ya La Liga dhidi ya Real Sociedad hapo Agosti 21 baada ya kuumia Goti kwenye Fainali ya EURO 2016.
Ronaldo and Portugal team-mate Pepe were back at the club's base for a low-key sessionJana Jumanne Usiku, Real Madrid, bila ya Mastaa hao, ilitwaa UEFA SUPER CUP walipoifunga Sevilla 3-2 huko Norway. Ronaldo, who suffered a knee injury in the final of Euro 2016, spent some time in the gymHuko Spain, Msimu Mpya utafunguliwa na Barcelona na Sevilla kwa kucheza Mechi ya kugombea Super Cup hapo Agosti 14 huko Sevilla na kurudiana Siku 3 baadae huko Nou Camp.

LA LIGA yenyewe itaanza Wikiendi ya Agosti 19.