Sunday, August 14, 2016

FULL TIME: ARSENAL 3 v 4 LIVERPOOL, TIMU YA WENGER NAYO YAANZA VIBAYA LIGI! MASHABIKI WAJIULIZA USAJILI!


Uwanja wa Emirates Jijini London ulikuwa na sherehe ya Magoli baada ya Bao 7 kutumbukizwa wakati Liverpool walipovunja gundu la kushinda Mechi 1 tu Nyumbani kwa Arsenal walipotoka kwa Bao 1-0 na kushinda 4-3.

Hii ilikuwa ni Mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England kwa Arsenal na Liverpool iliyoacha cheche kubwa na mwishowe kuwakasirisha Mashabiki wa Arsenal waliochomoka polepole Uwanjani kwao na kuuacha mtupu mwishowe huku wakimlaani Meneja wao Arsene Wenger.
Arsenal walianza Mechi hii kwa kishindo kwa kukosa Penati iliyotolewa baada ya Beki wa Liverpool Moreno kumwangusha Theo Walcott na Walcott mwenyewe kupiga na Kipa Mignolet kuokoa.

Lakini Dakika 1 baadae Walcott alirekebisha na kuipa Arsenal Bao katika Dakika ya 31 ambalo lilisawazishwa na Philippe Coutinho katika Dakika za Majeruhi za Kipindi cha Kwanza.
Hadi Mapumziko, Arsenal 1 Liverpool 1.

1-1 Hadi mapumziko
Arsenal pia walikosa mkwaju wa penati