Sunday, August 14, 2016

FULL TIME: BOURNEMOUTH 1 v 3 MANCHESTER UNITED, IBRA NA ROONEY WAFANYA KWELI KUANZA MSIMU MPYA!

WAKICHEZA huko Vitality Stadium katika Mechi ya kwanza kabisa ya himaya mpya ya Jose Mourinho ya Ligi Kuu England, Manchester United waliitandika Bournemouth Bao 3-1 na kuamsha shangwe za Mashabiki wao kuimba 'Jose Mourinho' mwishoni.
Man United walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 40 baada ya pasi ndefu ya Anders Herrera kuwahi na Beki wa Bournemouth Simon Francis ambae alitoa nyuma kumrudishia Kipa wakeBoruc lakini Juan Mata kuinasa na Kipa Boruc kuokoa na kumgonga tena Simon Francis na kurudi tena kwa Mata aliefunga kilaini.
Bao hilo lilidumu Hadi Haftaimu.

Kipindi cha Pili Dakika ya 59 Kepteni Wayne Rooney akapiga Bao la Pili kwa Kichwa baada ya Krosi ya Valencia kuunganishwa fyongo na Anthony Martial na kumkuta Rooney aliemalizia hadi wavuni.
Bao la 3 la Man United lilipachikwa na Mchezaji Mpya Zlatan Ibrahimovic katika Dakika ya 64 na kuwa Bao lake la kwanza kwa Klabu yake mpya.
Adam Smith aliipa Bournemouth Bao lao pekee Dakika ya 64 na Mechi kwisha Bournemouth 1 Man United 3.
Mwishoni Man United walifanya mabadiliko kwa kumtoa Juan Mata na kumpa Mechi yabkwanza Henrikh Mkhitaryan na kisha akatolewa Anthony Martial na kuongizwa Morgan Schneiderlin nabkufuata Wayne Rooney na kuja Memphis Depay.


Manchester United Bao zake zimefungwa na Juan Mata dakika ya 40, Wayne Rooney dakika ya 59 na la tatu likifungwa na Zlatan Ibrahimovic katika dakika ya 64 huku bao la AFC Bournemouth likifungwa na Adam Smith dakika ya 69.

Mechi inayofuata kwa Man United ni ya Nyumbani kwao Old Trafford Ijumaa ijayo dhidi ya Southampton ikiwa ni Mechi ya Ligi Kuu Englandm
Ligi Kuu England inaendelea baadae Leo kwa mtanange mkali huko Emirates kati ya Arsenal na Liverpool na Jumatatu ipo Mechi 1 kati ya Chelsea na West Ham United huko Stamford Bridge.