Saturday, August 13, 2016

FULL TIME EPL: HULL CITY 2 v 1 LEICESTER CITY, MABINGWA WATETEZI WAANZA VIBAYA MSIMU! SNODGRASS AWANYOOSHA!


MSIMU MPYA wa Soka wa Ligi Kuu huko England umeanza Leo huko Kingston upon Hull, KCOM Stadimu, kwa Timu iliyopanda Daraja Hull City kuwakaribisha Mabingwa wa England Leicester City kwa kuwatandika Bao 2-1.
Safari hii Ligi hii haina tena Jina la Mdhamini na itajulikana rasmi kama Ligi Kuu tofauti na Msimu uliopita ilipoitwa Barclays Premier League kutokana na udhamini wa Barclays.
Hull City, ambao hawana Meneja wa kudumu baada ya Steve Bruce kuamua kuondoka na wapo chini ya Msaidizi wa zamani wa Sir Alex Ferguson, Mike Phelan, walienda Mapumziko wakiwa Bao 1-0 mbele kwa Bao ambalo lilifungwa Dakika za Majeruhi baada ya krosi ya Robert Snodgrass kupigwa Kichwa na Curtis Davies na Kipa wa Leicester Kasper Schmeichel kuokoa na Mpira kugombewa na Wachezaji Wawili wa Hull, Abel Hernandez na Adama Diomande, wote wakiwania kupiga Tikitaka na Mpira kutinga wavuni.

Hata hivyo, Bao hilo alipewa rasmi Adama Diomande.
Kipindi cha Pili Dakika ya 47 Mabingwa Leicester walisawazisha kwa Penati ya Riyad Mahrez iliyotolewa kufuatia Rafu ya Huddlestone kwa Gray ambayo hakika ilifanyika nje ya Boksi.

Hull City walikwenda 2-1 mbele katika Dakika ya 57 kwa Bao nzuri la Robert Snodgrass la Shuti la chini kufuatia kizaazaa Goli mwa Leicester kilicholetwa na Krosi ya Ahmed Elmohamady na kuokolewa fyongo na Fulbeki Danny Simpson na kumdondokea Snodgrass aliemaliza vizuri.
Hadi mwisho Hull City 2 Leicester City 1.

Robert Snodgrass akishangilia bao lake dakika ya 57 kipindi cha bao alilolifunga kwa shuti kaliDama Diomand√© bao la kwanza dakika ya  (45'+1') kafunga.
Robert Snodgrass dakika ya (57') Huku bao la Leicester City ambao ni Mabingwa watetezi likifungwa kwa mkwaju wa penati na Riyad Mahrez