Saturday, August 27, 2016

FULL TIME: HULL CITY 0 vs 1 MANCHESTER UNITED, RASHFORD AFANYA MAAJABU DAKIKA ZA LALA SALAMA!! JOSE MOURINHO SHANGWE UGENINI!


Manchester United wameendelea na ushindi wa Asilimia 100 tangu Msimu Mpya wa LIGI KUU ENGLAND, EPL, kuanza kwa Leo kushinda Ugenini huko KCOM Stadium kwa Bao la Marcus Rashford la Dakika ya 92 na kuwapa ushindi wa 1-0 dhidi ya Hull City waliojenga Ukuta imara kwa Dakika 90 lakini kubomolewa mwishoni.

Bao hilo lilikuja baada ya Dakika 90 kwisha na bango kuashiria Dakika 4 za Nyongeza na kazi njema ya Kepteni Wayne Rooney kumtambuka Elmohamady na kupenyeza Pasi ya chini na Kijana Rashord kuunganisha na kutikisa wavu Dakika ya 92.
Hull City, ikiwa chini ya Kepteni wa zamani wa Man United Steve Bruce, ilipanda Daraja Msimu huu kurejea EPL lakini Bruce akabwaga manyanga baada ya kutofautiana na Wamiliki wake na Timu kuwa chini ya Mike Phelan ambae alikuwa Msaidizi wa Sir Alex Ferguson huko Old Trafford kwa Miaka mingi.


Mourinho hakubadilisha Kikosi chake kwa Mechi 3 za EPL lakini, wakishambulia bila mafanikio kwenye Mechi ilitokumbwa na Mvua kubwa, akalazimika kuwatoa Martial na Mata na kuwaingiza Mkhitaryan na Rashford na kuleta uhai.
EPL itaendelea tena kesho kwa Mechi 2 na kisha kupisha Mechi za Kimataifa kwa Wiki 2 na Mechi inayofuata ni Manchester Dabi kati ya Man United na Man City ndani ya Old Trafford.
Meneja wa Hull
VIKOSI:
Man Utd:
De Gea, Valencia, Bailly, Blind, Shaw, Fellaini, Pogba, Mata, Rooney, Martial, Ibrahimovic.
Subs: Smalling, Young, Rashford, Romero, Ander Herrera, Mkhitaryan, Schneiderlin.
 

Hull City
Hull:
Jakupovic, Elmohamady, Livermore, Davies, Robertson, Meyler, Huddlestone, Clucas, Snodgrass, Hernandez, Diomande.
Subs: Maguire, Kuciak, Maloney, Bowen, Olley, Clackstone, Hinchliffe.