Sunday, August 21, 2016

FULL TIME, LA LIGA: REAL SOCIEDAD 0 v 3 REAL MADRID

Gareth Bale (2')
Marco Asensio (40')

WAKICHEZA huko Estadio Municipal de Anoeta, Donostia-San Sebastián, Real Madrid, bila Staa wao Cristiano Ronaldo, wamefanikiwa kushinda 3-0 walipocheza na Real Sociedad kwenye Mechi yao ya kwanza ya Msimu mpya wa La Liga huko Spain.
Real walipata Bao Dakika ya Kwanza tu tangu Gemu kuanza Gareth Bale alipofunga kwa Kichwa akiunganisha Krosi safi ya Dani Carvajal kilichomshinda Kipa Rulli.
Real walipata Bao lao la Pili Dakika ya 40 kupitia Kijana wao Marco Asensio aliefunga kifundi baada ya kupokea pasi ndefu ya Raphael Varane.
Dakika ya 94, ikiwa ni mwisho wa Dakika 4 za nyongeza, Gareth Bale alifunga Bao lakeb la Pili na la 3 kwa Real alipopokea pande zuri toka kwa James Rodriguez na kumzunguka Kipa Rulli.