Monday, August 15, 2016

FULL TIME: CHELSEA 2 vs 1 WEST HAM UNITED, DIEGO COSTA AAMUSHA SHANGWE DARAJANI DAKIKA ZA LALA SALAMA KWA KUIPA BLUES BAO LA USHINDI!

Costa aokoa jahazi darajani leo dakika za majeruhi!!Diego Costa dakika ya (89') alifunga bao na kuipa bao la ushindi Blues kwa bao 2-1.
BAO la Dakika ya 89 la Diego Costa limewapa ushindi Chelsea katika Mechi yao ya kwanza ya Msimu mpya wa Ligi Kuu England chini ya Meneja mpya Antonio Conte walipoifunga West Ham Bao 2-1 Uwanjani Stamford Bridge.
Chelsea walitangulia kufunga katika Dakika ya 47, Kipindi cha Pili, kwa Penati iliyotolewa kufuatia Michail Antonio kumchezea Rafu Cesar Azpilicueta.
West Ham walisawazisha Dakika ya 77 kupitia James Collins lakini Chelsea wakanyakua ushindi kwa kupitia Costa aliepiga kutoka Mita 20.
Hata hivyo Costa alinusurika kuendelea kwenye Mechi hii hadi wakati huo kwani alilambwa Kadi ya Njano mapema na kisha kubahatika kutopewa Kadi ya pili baada ya kumkwangua Mguuni Kipa Adria.

West Ham walisawazisha bao kupitia kwa James Collins' dakika ya 77Eden Hazard dakika ya 47 kipindi cha pili alipachika bao la kwanza kwa mkwaju wa penati na kuifanya Chelsea kuongoza kwa bao 1-0 dhidi ya West Ham United.Hadi mapumziko Chelsea 0 West Ham United 0