Thursday, August 25, 2016

MAN CITY YAMSAINI KIPA BRAVO KWA MIAKA 4

Manchester City wamekamilisha kumsaini Kipa Claudio Bravo kutoka Barcelona kwa Dau ambalo halikutajwa.
Bravo, Raia wa Chile mwenye Miaka 33, amesaini Mkataba wa Miaka Minne na City ambao wako chini ya Meneja Pep Guardiola.

Bravo ndie alikuwa Kipa Namba Wani wa Barcelona tangu ajiunge nao Mwaka 2014 akitokea Real Sociedad lakini Mabingwa hao wa Spain sasa wamemruhusu kuondoka baada ya kumpata Kipa Jasper Cillessen aliekuwa Ajax Amsterdam.

Kutua kwa Bravo sasa kunaashiria mwisho wa Kipa wa England Joe Hart ambae ameidakia Klabu hiyo Mechi 348 lakini Msimu huu, katika Mechi zao 3 za kwanza, alipigwa Benchi na Golini kuwekwa aliekuwa rizevu wake Willy Caballero.
Sasa Hart, mwenye Miaka 29, anaweza kuwa Kipa Nambari 3 nyuma ya Bravo na Caballero akibakia Klabuni hapo.