Friday, August 5, 2016

MCHEZAJI BORA ULAYA NI BALE, GRIEZMANN AU RONALDO?

WACHEZAJI WAWILI wa Real Madrid, Gareth Bale na Cristiano Ronaldo, na mmpja wa Atlético Madrid', Antoine Griezmann, ndio waliopenya kufikia Fainali ya kugombea Tuzo ya UEFA ya Mchezaji Bora wa Ulaya kwa Msimu wa 2015/16.
Habari hizo zimetangazwa hivi punde na UEFA ambapo Watatu hao watapigiwa Kura hapo Alhamisi Agosti 25 huko Monaco wakati wa kuendesha Droo ya Kupanga Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI ili kumpata mmoja ambae ndie atazoa Tuzo ya UEFA ya Mchezaji Bora wa Ulaya kwa Msimu wa 2015/16.

Washindi waliopita wa Tuzo hii ni Lionel Messi (2011, 2015), Andrés Iniesta (2012), Franck Ribéry (2013) na Ronaldo (2014).

Kama ilivyo kawaida ya Tuzo hii, Wanahabari kutoka Nchi 55 Wanachama wa UEFA ndio Wapigaji Kura ambapo kila mmoja huteua Wachezaji wake Watano Bora na yule ambae ana Pointi nyingi ndio ameingia kwenye Fainali ya hao Watatu wa mwisho.

Watatu walioingia Fainali:
Gareth Bale (Real Madrid & Wales)
Antoine Griezmann (Atlético Madrid & France)
Cristiano Ronaldo (Real Madrid & Portugal)

Nafasi nyingine:
4 Luis Suárez (Barcelona & Uruguay) – 29 points
5 Lionel Messi (Barcelona & Argentina) – 25
6 Gianluigi Buffon (Juventus & Italy) – 19
7 Pepe (Real Madrid & Portugal) – 9
8 Manuel Neuer (Bayern München & Germany) – 6
9 Toni Kroos (Real Madrid & Germany) – 5
10 Thomas Müller (Bayern München & Germany) – 2: