Monday, August 1, 2016

MO KUIMILIKI SIMBA?

MKUTANO MKUU wa Wanachama wa Simba uliofanyika Bwalo la Maofisa wa Jeshi la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam Leo wameafika mabadiliko ya Katiba yao ili Klabu ijiendeshe Kikampuni kwa kuuza Hisa huku mlengwa mkubwa akiwa ni Mohamed Dewji, maarufu kama MO, ambae ni Rais wa Kampuni ya Mohamed Enterprise Limited, MeTL, ambae Juzi alitangaza kujikita na kuwekeza Simba ikiwa watakubalika.

Hii Leo, Rais wa Simba Evans Aveva, wameridhia mapendekezo hayo na kinachofuata ni kuweka utaratibu kwa Kamati teule kupitia Mfumo huo mpya na kisha mapendekezo kupelekwa Kamati Kuu kuchambua na hatimaye kurudishwa tena kwa Wanachama kutoa uamuzi.Mohamed Dewji, maarufu kama MO, ambae ni Rais wa Kampuni ya Mohamed Enterprise Limited, MeTL, Jumapili atatua mbele ya Mkutano wa Wanachama wa Klabu hiyo huko Mesi ya Maafisa wa Polisi, Oyster Bay Jijini Dar es Salaam kuwasilisha na kutaka ridhaa yao ya kununua Hisa Asilimia 51 za Klabu hiyo huku akiwekeza Kitita cha Shilingi Bilioni 20.

Akielezea mpango wake huo, MO, ambae aliwahi kuwa Mbunge wa Singida Mjini wa CCM, amesema Bilioni 20 zitawekwa kwenye Akaunti maalum Benki ambazo baada ya Miaka Mitano zitazaa Faida ya Shilingi Bilioni 3.5.

Pia, Kijana huyo Tajiri mkubwa Barani Afrika, ameeleza kuwa ataweka Bajeti ya Mwaka ya Shilingi Bilioni 5.5 kutoka ile ya Bilioni 1.2 ya sasa ambapo Bilioni 4 ni za kuendesha shughuli za Klabu ikiwa ni pamoja na kununua Wachezaji wakati Bilioni 1.5 zitakwenda kwenye shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuendeleza Uwanja wao wa Mazoezi huko Bunju na Programu za Timu za Vijana.

Kuhusu Uwanja wa Bunju, MO ameeleza atatumia Shilingo Bilioni 5 kuujenga uwe wa kisasa katika kipindi cha Miaka cha Mitano baada ya kutwaa Hisa za Asilimia 51 za Klabu ya Simba.

MO alishawahi kuwa Mfadhili wa Simba kati ya Miaka ya 1999 na 2005 na kuleta mafaniko makubwa ikiwa ni pamoja kuifikisha hatua ya Makundi ya CAF CHAMPIONS LIGI Mwaka 2003 baada ya kuwabwaga waliokuwa Mabingwa wa Afrika Zamalek ya Misri.