Friday, August 5, 2016

MOURINHO AONGEA: WENGER, KLOPP NI ‘WAKOSEFU WA MAADILI’, KUMSAINI KIUNGO BORA MUDA WOWOTE SASA!

LEO Meneja wa ManchesterUnited Jose Mourinho alizungumza na Wanahabari kuelekea Mechi yao ya Jumapili huko Wembley, London ya Kufungua Pazia Msimu Mpya wa 2016 dhidi ya Mabingwa wa England Leicester City ya kugombea Ngao ya Jamii.

Mbali ya kuzungumzia kuhusu Kikosi chake kwa ajili ya Mechi hiyo, Mourinho pia aliwajibu Meneja wa Arsenal Arsene Wenger na wa Liverpool Jurgen Klopp ambao waliponda jitihada za Man United kumsaini Kiungo wa Juventus Paul Pogba kwa Dau la Rekodi ya Dunia la Pauni Milioni 100.
Mourinho amedai kauli za Wenger na Klopp ni kukiuka maadili na ameeleza: “Kuna vitu nikifanya nasemwa ni kinyume cha maadili, wengine wakifanya ni sawa!”

Akigusia kuwa atamsaini Kiungo Bora ndani ya Siku kadhaa zijazo, Mourinho ameeleza: “Tuna Wachezaji 22. Tuakuwa na 23. Pogba ni Mchezaji wa Juve hadi ambapo rasmi sio. Soko linafungwa Agosti 31. Tunajaribu kukamilisha kabla Agosti 14!”
Wakati Wenger akidai kumsaini Mchezaji kwa Pauni Milioni 100 ni ‘wehu’, Klopp alidai asingefanya hivyo hata kama angekuwa na Fedha zisizokuwa na kikomo.

Kuhusu maendeleo yake na Mazoezi ya Kikosi chake, Mourinho amesema kuwa Timu yake ni tofauti na ile ya Meneja aliepita Louis van Gaal.
Amesema: “Ni ngumu kubadili mwelekeo wa Wachezaji baada ya kazi za Miaka Miwili lakini tunajaribu sana kuwabadili. Pole pole Timu hii itakuwa Timu yangu”
Kuhusu Ngao ya Jamii, Mourinho amesema: “Nadhani hii ni spesho waliokuwepo Msimu uliopita, ina maana kwao. Kucheza kwenye Ngao ya Jamii ni lazima uwe Bingwa au umetwaa FA CUP. Na wao walishinda FA CUP. Ni wazi tutajaribu kubeba Ngao ya Jamii!”

Pia Mourinho alieleza mipango yake ya kutumia Wachezaji wote 6 wa Akiba wanaoruhusiwa kucheza Mechi hiyo ya Ngao ya Jamii ili kuwapa nafasi Wachezaji zaidi Kikosini mwake.

Kwa upande wa Majeruhi, Mourinho ametoboa kuwa Chris Smalling na Tim Fosu-Mensah sasa wapo fiti na wapo mazoezini.


Arsene Wenger na Jose Mourinho wakipeana MkonoKlopp