Saturday, August 6, 2016

NDANI YA DSTV COMMUNITY SHIELD, LEICESTER CITY vs MANCHESTER CITY

Community Shield
MECHI YA Ufunguzi Pazia wa Msimu Mpya wa Soka wa England ambapo Mabingwa wa England na wale waliobeba FA CUP hukutana kugombea Ngao ya Jamii itachezwa Jumapili Uwanjani Wembley Jijini London.
Mechi hii itawakutanisha Leicester City ambao ni Mabingwa wa England na Manchester United Mabingwa wa FA CUP na itaanza Saa 12 Jioni Saa za Bongo.
Awali Taji hili lilikuwa likiitwa Ngao ya Hisani lakini sasa ni Ngao ya Jamii na hii ni mara 94 kushindaniwa na Mdhamini wake Mkuu ni McDonald ambao ni maarufu kwa Hoteli za Vyakula vya Hamburger Duniani kote.
Mara ya mwisho kukutana, Timu hizo zilitoka 1-1 Msimu uliopita kwenye Mechi ya Ligi Kuu England ambayo Leicester walitanguliwa kufungwa kwa Bao la Anthony Martial na kusawazisha kupitia Wes Morgan.

Siku moja baada ya Mechi hiyo, Leicester wakatwaa Ubingwa baada ya Wapinzani wao Spurs kutoka Sare na Chelsea huko Stamford Bridge.
Hilo lilikamilisha Msimu wa ajabu kwa Leicester baada ya Msimu mmoja uliopita, ule wa 2014/15 chupuchupu kunusurika kushushwa Daraja.
Lakini chini ya Meneja Claudio Ranieri Msimu wa 2015/16 walibadilika na kushangaza wengi kwa kutwaa Ubingwa wao wa kwanza katika Historia yao.
Ranieri ndie alikuwa Meneja wa Chelsea kabla Jose Mourinho hajatua huko kumbadili.

JE WAJUA?
-Man United wametwaa Ngao ya Jamii mara 20, ikiwa ni mara 5 zaidi ya Timu inayowafuata [Liverpool mara 15].