Wednesday, August 17, 2016

NGAO YA JAMII: AZAM FC YAICHAPA YANGA KWA PENATI 4-1

Washindi wa Pili wa Ligi Kuu Vodacom AZAM FC Leo wamefuta mwiko wa kubwagwa na Mabingwa wa Ligi Kuu Vodacom Yanga kwenye Mechi ya kufungua pazia Msimu mpya ya kugombea Ngao ya Jamii baada ya kuibuka kidedea kwa Mikwaju ya Penati 4-1 kufuatia Sare ya 2-2 katika Dakika 90.

Leo ni mara ya 4 mfululizo kwa Yanga na Azam FC kukutana kwenye Ngao ya Jamii na mara 3 zilizopita Yanga walibuka kidedea kwa Mwaka 2013 Yanga kushinda 1-0, Mwaka 2014 kushinda 3-0 wakati Mwaka Jana 2015 pia Yanga kuibuka kidedea kwa Mikwaju 8-7 ya Penati kufuatia Sare ya 0-0 katika Dakika 90.

Hi Leo Yanga walikwenda mbele 2-0 hadi Mapumziko kwa Bao za Donald Ngoma za Dakika za 20 na 22 lakini Kipindi cha Pili Azam FC wakajikongoja na kufunga Bao Dakika ya 74 kupitia Kapombe na kusawazisha Dakika ya 89 kwa Penati ya John Bocco Penati ambayo ilitolewa kwa madai Mchezaji wa Yanga aliunawa Penati.

Dakika 90 zilimalizika kwa Sare ya 2-2 na ikaja Mikwaju ya Penati Tano Tano na Azam FC kushinda Penati 4-1.

Kwenye Penati hizo, Yanga walikosa Penati 2 zilizopigwa na Hassan Kessy na Niyonzima huku Dida akifunga wakati Azam FC walifunga Penati zao zote 4 zilizopigwa na John Bocco, Himid Mao, Kapombe na Kipre Balou.

Sasa Ligi Kuu Vodacom itaanza Wikiendi lakini Mabingwa Watetezi Yanga watachelewa kuanza na watacheza Mechi yao ya kwanza Agosti 28 kwa kuwa Nyumbani dhidi ya African Lyon wakati Azam FC wakianza pia Nyumbani na hao hao African Lyon hapo Jumamosi Agosti 20 ambayo ndiyo Siku ya kwanza kabisa ya Ligi.

VIKOSI VILIVYOANZA:
AZAM FC:

Manula, Gambo, Kangwa, Mwantika,
Kapombe, Mao, Mugiranezi, Abubakar, Bocco, Idd, Singano

YANGA:
Munishi, Mwinyi, Kessy, Bossou, Twite, Kamusoko, Makapu, Niyonzima, Tambwe, Ngoma, Mahadhi

REFA: Ngole Mwangole [Mbeya]