Saturday, August 6, 2016

NGAO YA JAMII: JUMAPILI HAPATOSHI! LEICESTER CITY vs MAN UNITED, WEMBLEY

MECHI YA Ufunguzi Pazia wa Msimu Mpya wa Soka wa England ambapo Mabingwa wa England na wale waliobeba FA CUP hukutana kugombea Ngao ya Jamii itachezwa Jumapili Uwanjani Wembley Jijini London.

Mechi hii itawakutanisha Leicester City ambao ni Mabingwa wa England na Manchester United Mabingwa wa FA CUP na itaanza Saa 12 Jioni Saa za Bongo.

Awali Taji hili lilikuwa likiitwa Ngao ya Hisani lakini sasa ni Ngao ya Jamii na hii ni mara 94 kushindaniwa na Mdhamini wake Mkuu ni McDonald ambao ni maarufu kwa Hoteli za Vyakula vya Hamburger Duniani kote.

NINI MAMENEJA WAMESEMA:
-MAN UNITED: Jose Mourinho:

"Leicester sio mazoezi. Nadhani hii ni spesho waliokuwepo Msimu uliopita, ina maana kwao. Kucheza kwenye Ngao ya Jamii ni lazima uwe Bingwa au umetwaa FA CUP. Na wao walishinda FA CUP. Ni wazi tutajaribu kubeba Ngao ya Jamii!”

-LEICESTER CITY: Claudio Ranieri:
“Mameneja wote wanataka kucheza Wembley. Ni Uwanja maarufu Duniani. Nishahau nini kimetokea Msimu uliopita. Mkazo wangu ni Msimu huu mpya!”

Hali za Timu 

Mabeki wa Manchester United Chris Smalling na Timothy Fosu-Mensah, ambao walikuwa Majeruhi sasa wako fiti na huenda wakashiriki Mechi hii.

Wachezaji wapya wa Man United Zlatan Ibrahimovic, Henrikh Mkhitaryan na Eric Bailly huenda nao wakaanza Mechi hii.

MAN UNITED-Timu itatokana na Kikosi hiki:
De Gea, Romero, Bailly, Jones, Rojo, Darmian, Fosu-Mensah, Valencia, Smalling, Blind, Shaw, Carrick, Herrera, Schneiderlin, Fellaini, Lingard, Young, Mata, Mkhitaryan, Depay, Martial, Rooney, Rashford, Ibrahimovic.

Kwa upande wa Leicester City, Wachezaji wao wapya Ahmed Musa, Papy Mendy na Luis Hernandez huenda wakaanza pamoja na wengine wapya Ron-Robert Zieler na Bartosz Kapustka.

LEICESTER CITY:
Schmeichel, Zieler, Chilwell, Schlupp, Morgan, Hernandez, Wasilewski, Huth, Fuchs, Simpson, Kapustka, Gray, Amartey, King, Mendy, Drinkwater, James, Albrighton, Mahrez, Ulloa, Okazaki, Musa, Vardy.

REFA: CRAIG PAWSON