Friday, August 5, 2016

OLIMPIKI RIO 2016: BRAZIL0 v 0 SOUTH AFRICA, WAANZA KWA SARE WENYEJI!

Mechi za Soka kwa Wanaunme katika Michezo ya Olimpiki ya Mwaka 2016 zilianza huko Nchini Brazil, maarufu kama OLIMPIKI RIO 2016, na Wenyeji Brazil kutoka 0-0 na South Africa.
Mechi hiyo ya Kundi A ilichezwa huko Mané Garrincha Stadium, Brasilia na Washabiki kuizomea Brazil, iliyoongozwa na Neymar, kwa Matokeo hayo.
Mechi nyingine ya Kundi A ilikuwa pia Sare ya 0-0 kati ya Iraq na Denmark.
Kwenye Soka la Wanaumew zipo Timu 16 za Wanaume na yapo Makundi Manne ya Timu 4 kila moja na Mechi hizo kuchezwa katika Miji 6 ya Nchini Brazil ambayo ni Rio de Janeiro, Belo Horizonte, Brasília, Salvador, São Paulo na Manaus.


Ukikiondoa Kiwanja kiitwacho Estádio Olímpico João Havelange Mjini Rio de Janeiro, Viwanja vyote vilivyobaki vitakavyotumika kwa Mechi hizi pia vilitumika kwa Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 2014.