Wednesday, August 3, 2016

OLIMPIKI RIO 2016: SOKA KUANZA LEO!

MICHEZO ya Olimpiki ya Mwaka 2016 huko Nchini Brazil, maarufu kama OLIMPIKI RIO 2016, inaanza rasmi Ijumaa hii kwa Sherehe rasmi za Ufunguzi lakini kwa upande wa Soka kwenye Michezo hiyo Mechi zake zitaanza Leo kwa Mechi ya Makundi ya Wanawake kati ya Sweden na South Afrika.
Mechi za Makundi kwa Wanaume zitaanza Alhamisi wakati Denmark watakapocheza na Iraq.

Sababu pekee inayofanya Soka ianze mapema kwenye Michezo hiyo ni sababu za Ratiba tu.

Kwenye Soka zipo Timu 16 za Wanaume na Timu 12 kwa Wanawake na hivyo Jumla zipo Mechi 58 zitakazochezwa katika Siku 12 za Michezo hiyo huku Siku 6 ni za Mapumziko.

Kwa upande wa Wanaume, yapo Makundi Manne ya Timu 4 kila moja na Mechi hizo kuchezwa katika Miji 6 ya Nchini Brazil ambayo ni Rio de Janeiro, Belo Horizonte, Brasília, Salvador, São Paulo na Manaus.

Ukikiondoa Kiwanja kiitwacho Estádio Olímpico João Havelange Mjini Rio de Janeiro, Viwanja vyote vilivyobaki vitakavyotumika kwa Mechi hizi pia vilitumika kwa Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 2014.

MAKUNDI:
Wanaume

KUNDI A: Brazil, South Africa, Iraq, Denmark
KUNDI B: Sweden, Colombia, Nigeria, Japan
KUNDI C: Fiji, South Korea, Mexico, Germany
KUNDI D: Honduras, Algeria, Portugal, Argentina

Wanawake
KUNDI E:
Brazil, China, Sweden, South Africa
KUNDI F: Canada, Australia, Zimbabwe, Germany
KUNDI G: USA, New Zealand, France, Columbia

Mashindano ya Soka ya Michezo ya Olimpiki hushirikisha Timu za Vijana wa chini ya Miaka 23 waliozaliwa Januari Mosi, Mwaka 1993 au baada ya hapo lakini kila Timu ruksa kuchezesha Wachezaji Watatu wa Umri wa juu zaidi ya hapo.

Timu ya Wenyeji Brazil itaongozwa na Supastaa wao mkubwa, Straika wa FC Barcelona ya Spain, Neymar.

Washindi Wawili wa juu wa kila Kundi watatinga Robo Fainali.
Ratiba
Wanaume
Makundi
Alhamisi Agosti 4
KUNDI A

Mané Garrincha Stadium, Brasilia
Iraq v Denmark

KUNDI D
Olympic Stadium, Rio De Janeiro
Honduras v Algeria
KUNDI A
Mané Garrincha Stadium, Brasilia
Brazil v South Africa

KUNDI C
Fonte Nova Arena, Salvador
Fiji v Korea Republic

KUNDI D
Olympic Stadium, Rio De Janeiro
Portugal v Argentina

KUNDI B
Amazônia Arena, Manaus
Sweden v Colombia

KUNDI C
Fonte Nova Arena, Salvador
Mexico v Germany

KUNDI B
Amazônia Arena, Manaus
Nigeria v Japan

Jumapili Agosti 7

KUNDI C

Fonte Nova Arena, Salvador

Fiji v Mexico

KUNDI D

Olympic Stadium, Rio De Janeiro

Honduras v Portugal

KUNDI C

Fonte Nova Arena, Salvador

Germany v Korea Republic

KUNDI D

Olympic Stadium, Rio De Janeiro

Argentina v Algeria

KUNDI B

Amazônia Arena, Manaus

Sweden v Nigeria

KUNDI A

Mané Garrincha Stadium, Brasilia

Denmark v South Africa

KUNDI B

Amazônia Arena, Manaus

Japan v Colombia

KUNDI A

Mané Garrincha Stadium, Brasilia

Brazil v Iraq

Jumatano Agosti 10

KUNDI D

Mineirão, Belo Horizonte

Algeria v Portugal

KUNDI D

Mané Garrincha Stadium, Brasilia

Argentina v Honduras

KUNDI C

Mineirão, Belo Horizonte

Germany v Fiji

KUNDI C

Mané Garrincha Stadium, Brasilia

Korea Republic v Mexico

KUNDI B

Corinthians Arena, Sao Paulo

Colombia v Nigeria

KUNDI B

Fonte Nova Arena, Salvador

Japan v Sweden

KUNDI A

Fonte Nova Arena, Salvador

Denmark v Brazil

KUNDI A

Corinthians Arena, Sao Paulo

South Africa v Iraq

Robo Fainali

Jumamosi Agosti 13

-Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B [Sao Paulo]

-Mshindi Kundi C v Mshindi wa Pili Kundi D [Belo Horizonte]

-Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A [Salvador]

-Mshindi Kundi D v Mshindi wa Pili Kundi C [Brasilia]

Nusu Fainali

Jumatano Agosti 17

-Rio De Janeiro: Mechi 28 v Mechi 27

-Sao Paolo: Mechi 26 v Mechi 25

Mshindi wa 3-Medali ya Shaba

Jumamosi Agosti 20

- Belo Horizonte:

Fainali

Jumamosi Agosti 20